*Wadai marehenu hakuwajali.
*Mwili washinda ndani ndugu watokomea.
*Balozi wa mtaa aokoa jahazi.
******
Habari kamili na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Familia ya
Edson Mbembela wa Nzovwe imejikuta ikiingia matatani baada ya
kuutelekeza mwili wa ndugu yao aliyekuwa mjane ambaye aliolewa na
mwanawe Ebnesa Mbembela aliyefariki mwaka 2005.
Marehemu
alikuwa akiishi mtaa wa Iyela jijini Mbeya na kufariki Mei 7 mwaka huu
majira ya saa nene mchana katika nyumba inayomilikiwa na Bwana Giseon
Kyebeleka, ambaye ni Askari magereza wa Chuo cha Magereza Kiwira mkoani
Mbeya.
Aidha inadaiwa
marehemu alifariki kutokana na maumivu ya kichwa kutokana na kupiga
nondo hivi eneo la Sido jijini hapa alipokuwa anarejea nyumbani majira
ya usiku.
Balozi wa Mtaa
huo Bwana Lwitiko Mwanyingili amesema marehemu alijaaliwa kupata watoto
wanne, ambapo wawili walikuwa wakiishi na marehemu kabla ya kifo chake
na mara baada ya kufariki walimtafuta baba mkwe Bwana Edson Mbembela na
kumtaarifu juu ya kifo cha mkwewe.
Baada ya
taarifa hizo Bwana Mbembela na mkewe Bi Maria Mbembela (70) walidai
hawako tayari kuzika kwa vile marehemu hakumuuguza marehemu mmewe
aliyefariki mwaka 2005 na pia alikuwa hawatembelei nyumbani.
Aidha Baba mkwe huyo aliagiza ndugu wa marehemu huyo wamzike na baada ya mazishi aletewe watoto hao kwa ajili ya kuwatunza.
Uapnde wa pili
wa ndugu wa marehemu nao walikataa kumzika wakidai kuwa binti yao
walimuoza kwa ukoo wa Mbembela na pia marehemu alikuwa hawatembelei
hivyo hawana haki ya kumzika.
Balozi
Mwanyingili aliamua kumtaarifu Mwenyekiti wa mtaa wa Iyela Bwana Japhet
Mwangonele ambapo alizikutanisha pande zote mbili bila mafanikio na hata
alipotoa taarifa Kituo cha Polisi Mwanjelwa nao hawakuwa nala kufanya.
Naye, Mchungaji
wa Kanisa la Church of God Solomon Mwashoma, amesema amesikitishwa sana
na tukio hilo na kumhukumu marehemu kwani huo ni ukatili.
Mchungaji huyo
ameenda mbali sana kwa kusema si vema kuwanyanyasa wajane na hii ni
hatari zaidi kwa jamii ya kitanzania na kuwaasa watu wenye tabia kama
hizo kuacha mara moja.
Pia viongozi
mbalimbali wa mtaa wameaswa kutowapokea watu bila kuwa na barua za
mahali walikotoka kwani iliwachukua muda ilikuzipata koo zote mbili
kutokana na marehemu kuhamia mtaani hapo wiki mbili zilizopita.
Hata
hivyo baada ya kushindwa kupatikana kwa muafaka balozi huyo wa mtaa
Bwana Mwanyingili alitoa shilingi 25,000 kwa ajili ya kuupeleka mwili wa
marehemu Hospitali ya rufaa Mbeya kusubiri maafikiano ya ndugu wa pande
zote mbili waishio Nzovwe.
No comments:
Post a Comment