Pages

Tuesday, May 8, 2012

GEREZA LA RUJEWA LATEMBELEWA NA UMOJA WA WANAWAKE WA KANISA LA MOROVIAN.

Na Bosco Nyambege ,Rujewa
 Umoja wa Wanawake kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi katika Ushirika wa Yerusalemu iliyopo Mkoani Mbeya wamezuru Gereza la Rujewa iliyopo Wilayani Mbarali hivi karibuni.
 
Ziara hiyo iliambatana na kutoa zawadi kwawafungwa wote wa Gereza hilo kama katoni nane za sabuni,mafuta ya kujipaka yaani lotion na mafuta ya mgando dazani 40 ikiwa pamoja na chumvi .
 
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake ushirika wa yerusalemu Eda Kapora alipohojiwa kuhusiana na suala hilo alidai kuwa hiyo ni moja ya huduma  wanayofanya wanawake amabyo ni dhamana ya mzigo wa liopewa na mwenyezi mungu wa kutembelea wajane  ikiwa pamoja na wafungwa ,watoto yatima  na watu wanaoishi katika mazingira magumu   .
 
Kapora aliongeza kuwa kwani mpaka sasa wamekwisha kutembelea vituo mbalimbali  kama vile watoto yatima ,nyumba za wajane  watu wanaoishi ktika mazingira magumu n a ka sasa wameanza kuzuru katika magereza .
 
Kwa upande wake mchungaji mlezi wa kanisa hilo Peter Mwambalaswa alisema kuwa dini iliyo safi n kutazama wafungwa  ,wajane  na wanaoishi katika mazingira magumu .
 
Hata hivyo alisema kuwa ni muhimu kwa kanisa lolote kutambua wajibu mkubwa waliopewa na mwenyezi mungu juu ya kuhudumia wale wanaowazunguka na wale walio mbali nao wanaohitaji msaada wao .
 
Vilevle alsema kuwa ni vyema askari magereza wanaofanya kazi ya kuwalinda wafungwa magerezani kutambua kwama wao ni wachungaji na mungu atawalipa kama watafanya yale wanaompendeza yeye .
 
 
Alison  Mwasile ambaye ni mchungaji wakanisa la Moravian Usharika wa Rujewa amewasihi wafungwa kuonesha ushirikiano wao mzuri baina  yao na mungu pindi wanapokuwa gerezani na pindi wanapokuwa wanatoka .
 
Mwasile alisema kuwa magerezani wapo walimu wazuri wa imanikwani hata kipindi cha yusufu alipfunga gerezani kuilikuwa na kusudi maalumu ambalo  mungu aliliweka  ndani yake .
 
Mmoja wa wafungwa amabaye jina lake hakutaka jina lake litajwe aliyaomba makanisa  na dini mbalimbali kuweza kuwaombea  kwani wapo walio magerezani hawana hatia  yeyote .
 
Kwa upande wake Askari wa Gereza hilo ambaye jina lake hakutaka litajwe katika gazeti hili alisema ujio wa makanisa  gerezani  kunapelekea wao kuona mwanga  katia maisha yao  kwani wanapata  mawazo mbalimbali  kutoka kwa watumishi wa mungu  kuhusiana na shughuli zao..
 
Alisema  kuwa  hata kwa  upande  wa wafungwa  ni furaha kubwa kuona watumishi wa mungu wanaokuja kuwatembelea maeneo hayo kwani  wanapata faraja  na matumani  katika  maisha  yao  hata wawapo  gerezani  .

No comments:

Post a Comment