Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mbeya mheshimiwa Dakta Mary Mwanjelwa mbunge wa viti maalum mkoa wa mbeya akiongea na wananchi wa mwanjelwa katika kiwanja cha sido, ambaye anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika Kongamano la Maombi la kuuombea Mkoa dhidi ya Vitendo viovu.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Kongamano la Maombi ya kuuombea Mkoa wa Mbeya, dhidi ya vitendo viovu vikiwemo vya upigaji nondo, kujichukulia sheria mkononi, uchunaji ngozi, mauaji ya albino, watoto na imani za kishirikina litafanyika leo katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari St Mary iliyopo Forest mpya jijini Mbeya.
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo anatarajiwa kuwa Mbunge wa viti Maalumu wa Mkoa wa Mbeya Dakta Mary Mwanjelwa, ambapo atafuatana na viongozi mbalimbali wa Serikali mkoani hapa.
Kongamano hilo limeratibiwa na Kipindi cha Faraja yako kinachorushwa kila siku kuanzia saa 11:00 alifajiri mpaka 12:30 asubuhi na saa 3:00 usiku mpaka 4:00 usiku katika kituo cha Kurushia matangazo cha Bomba FM redio, kupitia masafa ya 104.0 kilichopo mkoani hapa.
Aidha, baadhi ya vitendo vilivyotokea hivi karibuni mkoani hapa ni pamoja na kupingwa nondo Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Bwana Medrick Sanga, Aprili 10 mwaka huu wakati akienda katika studio za kurekodi muziki maarufu kwa jina la Mbeya Records iliyopo ndani ya Kanisa la KKKT Usharika wa Forest.
Hata hivyo mbali na tukio hilo watu kadhaa wamedaiwa kuuawa kwa imani za kishirikina na mwingina kuzikwa hai baada ya kuhusishwa kuwa ni mchawi na pia watoto wa shule kuanguka mara kwa mara wawapo mashuleni kwao.
No comments:
Post a Comment